SW/Prabhupada 0002 - Madman Civilisation



Lecture on SB 6.1.49 -- New Orleans Farm, August 1, 1975

Harikeśa: Ufasiri... "Kama vile mtu kwenye ndoto anatenda kulingana na udhiirisho wa mwili wake kwenye usingizi, au anakubali mwili wake kuwa yeye, Vile vile, anabaiani mwili alio nao wakati huu kuwa yeye, ambayo ilipatikana kwa sababu ya maisha yake iliyopita aitha iliyokuwa takatifu au yenye dhambi, na hawezi kujua kuhusu maisha yake iliyopita au ijayo." Prabhupāda:

yathājñas tamasā (yukta)
upāste vyaktam eva hi
na veda pūrvam aparaṁ
naṣṭa-janma-smṛtis tathā
(SB 6.1.49)

Huu ndio msimamo wetu. Hii ndio maendeleo yetu ya kisayansi, kuwa hatujui, "Nilichokuwa kabla ya maisha hii na ntakachokuwa baada ya maisha hii?" Maisha ni muendeleo. Haya ndio maarifa ya kiroho. Lakini hawajuwi ya kwamba maisha ni muendeleo pia. Wanafikiria, "Kwa bahati, nimepata maisha haya, na itamalizika baada ya kifo. Hakuna cha zamani, sasa au baadae. Tufurahie? Hii inaitwa ujingwa, tamasā, maisha isio kuwa na majukumu. Kwa hivyo ajñaḥ. Ajñaḥ inamaanisha, yule amabaye hana maarifa. Na nani hana maarifa? Sasa, tamasā. Waliyo kwenye hali ya ujinga. Kuna aina tatu za hali za kidunia: sattva, raja, tamas. Sattva-guṇa inamaanisha kila kitu kiko wazi, prakāśa. Kama vile sasa, mbingu imefunikwa na mawingu; jua haiko wazi. Lakini juu ya mawingu kuna jua, kila kitu kiko wazi. Na ikiwa kweneye mawingu haiko wazi. Vile vile, walio kwenye sattva-guṇa, kwao kila kitu kiko wazi, na walio kwenye tamo-guṇa, kila kitu ni ujinga, na wale walio kweneye mchanganyiko, ambao sio rajo-guṇa (sattva-guṇa) wala tamo-guṇa, wanaitwa rajo-guṇa. Guṇa tatu. Tamasā. Kwa huvyo wana shughulika na mwili huu tu, hawajali kitakacho fanyika, na ahajui alichokuwa hapo awali. Kuna mahali pengine imesemekana kuwa: nūnaṁ pramattaḥ kurute vikarma (SB 5.5.4). Pramattaḥ, kama vile wazimu. Hajui chanzo cha wazimu wake. Anasahau. Na kwa matendo yake, kitakacho tendeka baadaye, hajui. Wazimu.

Kwa hivyo huu ustaarabu wakisasa ni kama ustarabu wa mtu aliye na wazimu. Hawajui kuhusu maisha iliyopita, wala hawana hamu ya maisha ijayo. Nūnaṁ pramattaḥ kurute vikarma (SB 5.5.4). Na wamejawa na vitendo vya dhambi kwa sababu hawajui kuhusu maisha iliyopita. Kama tu mbwa. Mbona amekuwa mbwa? Hiyo hajui Na atakachopata baadaye? Kwa hivyo inawezekana kuwa mbwa alikuwa waziri mkuu katika maisha yake iliyopita, lakini anapopata maisha ya mbwa, anasahau. iyo pia ni athari ya māyā. Prakṣepātmikā-śakti, āvaraṇātmikā-śakti. Māyā ina nishati mbili. Ikiwa mtu amekuwa mbwa kwa sababu ya vitendo vyake vya dhambi katika maisha yake iliyopita, na akikumbuka kuwa, "Nilikuwa waziri mkuu, na sasa nimekuwa mbwa," hataweza kuishi. Kwa hivyo māyā inaziba maarifa yake. Mṛtyu. Mṛtyu inamaanisha kusahau kila kitu. Iyo inaitwa mṛtyu. Kwa hivyo tuna hisia hizi usiku na mchana. Usiku tunapota kuwa tuko kwenye mazingira tofauti au maisha tofautu, tunasahau mwili huu, kuwa "Nimelala chini. Mwili wangu umelala chini kwenye nyumba nzuri, kitanda kizuri." Hapana Tuseme anazurura mtaani au yuko juu ya mlima. Kwa hivyo anadhania, kwa ndoto, anadhania... Kila mmoja, tunajitambulisha kwa mwili huo. Tunasahau mwili tuliokuwa nayo. Hii ni ujinga. Kwa hivyo mafanilio ni wakati ambapo tunaendelea kuinuliwa kutoka kwa ujinga kwenye maarifa. Na tukijiweka ujingani, hatuta faulu. Hiyo ni kuharibu maisha. Kwa hivyo chama chetu cha Kṛṣṇa consciousness, kina muinuwa mtu kutoka kwa ujinga na kumweka kwenye maarifa. Hiyo ndiyo mpango wote wa maadiko ya Vedasi. Kumwokoa mtu. Kṛṣṇa anasema kwenye Bhagavad-gītā kuhusu waja- sio kwa watu wote- teṣāṁ ahaṁ samuddhartā mṛtyu-saṁsāra-sāgarāt (BG 12.7). Nyingine:

teṣāṁ evānukampārtham
aham ajñāna-jaṁ tamaḥ
nāśayāmy ātma-bhāva-stho
jñāna-dīpena bhāsvatā
(BG 10.11)

Kwa watu maalum, waja... Anakaa kwenye myoyo ya watu wote, Kṛṣṇa anamsaidia mja ambaye anajaibu kumwelewa. Anamsaidia. Wasio wafuasi hawajali... Wao ni kama wanyama- kula, kulala, kufanya ngono na kujikinga. Hwajali kamwe, kumwelewa Mungu au uhusiano wao naye. Kwao, wandhania kuwa Mungu hayuko, na Kṛṣṇa pia anasema, "Naam Mungu hayuko. We lala tu." Kwa hivyo sat-saṅga inahitajika. sat-saṅga, satāṁ prasaṅgāt. Kupitia mashirikiano wa waja, tunazindua udadisi wetu wa kutaka kumjua Mungu. Kwa hivyo vituo vina hitajika. Sio bure tunafungua vituo vingi. La. Ni kwa manufaa ya wanadamu wote.