SW/Prabhupada 0004 - Don't Surrender To Any Nonsense



Lecture on BG 10.2-3 -- New York, January 1, 1967

Njia ni... Hiyo pia imetajwa kwenye Bhagavad-gītā. Tad viddhi praṇipātena paripraśnena sevayā (BG 4.34). Ikiwa unataka kuelewa hiyo sayansi ya kiroho, basi ni lazima ufuate kanuni hii. Hiyo ni nini? Tad viddhi praṇipātena. Lazima ujisalimu. Vile vile namanta eva. Mpaka mtu awemtiifu, hawezi kujisalimu. Wapi? Praṇipāta. Mahali utakapompata mtu amabaye "Yeye ni...Huyu ndiye mtu ninayeweza kusalimu kwake"? Kwa hivyo inamaana kuwa lazima tufanye utafiti mdogo tutakapo salimu. Maarifa hayo, lazima uwe nayo. Usijisalimu kwa ujinga wowote. Ni lazima...Na hiyo maarifa ama ujinga utataburikana aje? Hiyo pia imetajwa kwa maandiko. hiyo imetajwa katika Kaṭha Upaniṣad. Tad viddhi praṇipātena pari... (BG 4.34). Katha Upinishad inasema tad-vijñānārthaṁ sa gurum evābhigacchet śrotriyaṁ brahma-niṣṭham [MU 1.2.12]. śrotriyam inamaanisha kuwa mtu yule anayefuata katika mfululizo wa nidhamu. Ni nini ushahidi kwamba huyo mtu anafuata mfululizo wa nidhamu? Brahma-niṣṭham. Brahma-niṣṭham inamaana huyo mtu anaamini Ukweli Mkuu Kabisa. Hivyo hapo lazima usalimu. Praṇipāta. Praṇipāta inamaana prakṛṣṭa-rūpeṇa nipātam, kabisa. ukimpata huyo mtu, basi jisalimu kwake. Praṇipāta.

na ujaribu kumtumikia, jaribu kumfurahisha ,na kumuuuliza maswali. hii itadhihirisha. lazima utafute huyo mtu alio na mamlaka na usalimu kwake. kujisalimisha kwake inamaanisha kujisalimisha kwa Mungu kwa sababu yeye ni mwakilishi wa Mungu. Lakini unaruhusiwa kuuliza maswali ,sio kupoteza wakati, ndio uelewe. hiyo inaitwa paripraśna. hizi ndio njia. hivyo kila kitu iko. tunafaa kufuata tu. lakini tusipofuata hii njia na tupoteze wakati wetu katika ulevi na uvumi na shughuli sisizonamaana, basi hiyo haiwezekani kabisa. Mtu hatawai elewa Mungu. kwa sababu Mungu hawezi eleweka hata na Mungu-mtu na watakatifu wakuu. nini juhudi zetu kidogo?

kwa hivyo hii ndio njia. na mtu akifuata, asammūḍhaḥ, asammūḍhaḥ,ukifuata kanuni hizi polepole kwa hakika, asammūḍhaḥ, bila shaka,ukifanya...hiyo ndio... Pratyakṣāvagamaṁ dharmyam. ukifuata utakujakujifahamu, "Ndio. Napata kitu." Sio kwamba uko kwa giza ,haufuati kama kipofu. Unapofuata kanuni, utakuja kufahamu. Kama vile unapokula chakula cha kuboresha , huwa unahisi kupata nguvu na njaa yako inaisha. Hauhutaji kuuliza mtu yeyote. Utahisi mwenyewe. vile vile, ukija kwa njia iliosahihi na ufuate kanuni zake ,utakuja kuelewa, "Ndio ,nafanya maendeleo." Pratyakṣa...katika sura ya tisa Krshna amesema pratyakṣāvagamaṁ dharmyaṁ susukham.

Na ni rahisi sana. Na unawezafanya kwa furaha. Na njia ni ipi? kuimba Hare Kṛṣṇa na kula kṛṣṇa-prasāda na kusoma Bhagavad-gītā,na kuskia sauti nzuri za kimziki. Ni ngumu sana? Ni ngumu sana? Sio hata kidogo. Hivyo kwa njia hii utakuwa asammūḍhaḥ. Hakuna mtu anaweza kukudanganya. lakini ukitaka kudanganywa kuna wadanganyifu wengi sana. Hivyo usitengeneze jamii ya wadanganyifu na wadanganywaji. Fuata mfumo wa paramparā kama inavyoelezwa katika maandiko ya veda ,kama ilivyopendekezwa na Kṛṣṇa. Jaribu kuifahamu kutoka kwa chanzo kilicho na mamlaka na kuitumia katika maisha yako. basi asammūḍhaḥ sa martyeṣu. Martyeṣu inamaana... Marya inamaana wale ambao watapitia kifo. Hao ni nani? hizi roho katika hali ya masharti, kutoka kwa Brahmā hadi kwa mchwa, wote ni martya. Martya inamaanisha kuna wakati watukufa. Hivyo martyeṣu. Miongoni mwa mwa binadamu watakaokufa yeye ndiye ana akili ya juu. Asammūḍhaḥ sa martyeṣu. Kwa nini? Sarva-pāpaiḥ pramucyate. Huyo mtu ako huru kutokana na adhari zozote za vitendo vya dhambi.

Katika ulimwengu huu, katika dunia hii, namaanisha kusema,kwa kujua ama kutojua, tunafanya dhambi kila wakati. Hivyo lazima tutoke katika adhari hizi. Na ni vipi kutoka? Hiyo pia imesemwa kwa Bhagavad-gītā. Yajñārthāt karmaṇo 'nyatra loko 'yaṁ karma-bandhanaḥ (BG 3.9). ukifanya matendo kwa ajili ya Kṛṣṇa...Yajña inaaminisha Viṣṇu au Kṛṣṇa. Ukitenda kwa ajili ya Kṛṣṇa pekee, basi unakua huru kutokana na majibu ya chochote kile. Śubhāśubha-phalaiḥ. huwa tunafanya matendo yenye heri au yenye balaa. Lakini wale waliokatika Ufahamu wa Kṛṣṇa na wanafanya vitendo hivyo, Hana uhusiano wowote na yale ya heri au balaa kwa sababu ako katika mguso na mwenye heri, Kṛṣṇa. hivyo hiyo sarva-pāpaiḥ pramucyate. Anafanywa huru kutokana na adhari za matendo ya dhambi. Hii ndio njia. Na tukifuata njia hii, mwishowe tutaweza kupatana na Kṛṣṇa Na maisha yetu itafanikiwa. Njia ni rahisi sana,na tunaweza, kila mtu anawezafuata. Asanteni sana.