SW/Prabhupada 1061 - Kwenye Bhagavad-gita mada muhimu ni kuelewa Haki kwa njia tano tofauti



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Bwana Krishna anasema, anaashuka, yadā yadā hi dharmasya glānir bhavati (BG 4.7), ili kuanzisha lengo halisi maishani wakati binaada anaposahau lengo halisi maishani, sababu ya kuwa na umbo la kibinaadam inaitwa dharmasya glāniḥ, usumbufu wa kimatendo kwa mwanaadamu. katika hiyo hali, kati ya binaadam wengi zaidi anayezinduka ni yule ambaye anazinduka katika roho ya kuelewa cheo chake kusudi ya mtu kama huyo basi hii Bhagavad-gītā imeongewa Ni kama tumemezwa na chui jike la ujinga, na kwasababu Bwana yu mwenye huruma kwa viumbe vyote sana sana kwa binaadam. Alinena Bhagavad-gītā, kumfanya rafikiye Arjuna kuwa mwanafunzi.

Arjuna kuwa mshiriki wa Bwana Krishna bila shaka hakuwa na ujinga wowote Lakini, alisababishwa kuwa mjinga katika uwanja wa vita wa Kurukṣetra ili aweze kumuliza Bwana mkuu maswali kuhusu matatizo ya maisha kusudi Bwana ayaeleze, ili kufaidi vizazi vijao vya binaadam kumwonyesha mpango wa maisha yake ili matendo yake ya fuate njia hiyo, ili maisha yake, dhamira yake kama mwanadamu iwe kamilifu.

Kwa hivyo kwenye Bhagavad-gītā, mada muhimu ni kuelewa Haki kwa njia tano tofauti, Haki ya kwanza, ni Mungu ni kumaanisha nini? hiyo ni somo ya kwanza ya sayansi ya kumjua Mungu. iyo sayansi imeelezwa hapa. Ijayo ni cheo halisi cha kiumbe, jīva. Īśvara na jīva. Mungu mkuu anajulikana kama īśvara.. Īśvara inamaana kuwa ni mtawala, na jīva,, viumbe ni watawaliwa Ki bandia nikisema kuwa sitawaliwi, niko huru, haitakuwa timamu. Kiube chochote kina tawaliwa kwa kila njia. anatawaliwa angalau kwenye hali yake isio kuwa huru maishani.

Kwa hiyo kwenye Bhagavad-gītā mada muhimu ni kumwelewa īśvara, mtawala mkuu na kuhusu viumbe watawaliwa, na prakṛti, maumbile ya dunia. Na ijayo ni muda, au kipindi cha uwepo wa ulimwengu mzima, au huu udhiirisho wa maumbile ya dunia, na kipindi cha muda, or muda uishie milele. na Karma. Karma inamaanisha vitendo. Kila kitu, ulimwengu mzima umejawa na vitendo tofauti. Sana sana viumbe wanahusika na vitendo tofauti. kwa hivyo ni lazima tujifunze kutoka kwa Bhagavad-gītā, kuhusu īśvara, yani Mungu ni kumaanisha nini, jīva, hivi viumbe ni nini, na prakṛti, ulimwengu ni nini, na vile inatawaliwa na wakati, na vitendo hivi ni nini?

Kati ya mada hizi tano kwenye Bhagavad-gītā, inafumbuliwa kuwa Mungu mkuu au Krishna au Brahman au Paramatma... unaweza kumwita kwa majina yoyote upendavyo. Lakini mtawala mkuu yuko. yeye ni mkuu zaidi kushinda wote. Viumbe vina sawiana kitabia na mtawala mkuu. kama vile, Bwana, mtawala mkuu, anaweza kutawala shughuli zote za ulimwengu na duniani, vile.. itaelezwa kwa sura zijazo kuwa dunia haiko huru. anatenda chini ya uongozi wa Mungu mkuu. Mayādhyakṣeṇa prakṛtiḥ sūyate sa-carācaram (BG 9.10). "Hii dunia inafanya kazi chini ya uongozi wangu," mayādhyakṣeṇa, "chini ya uongozi wangu"