SW/Prabhupada 1074 - Matatizo yote tunayopitia duniani - Ni kwa sababu ya mwili huu



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Mahali pengine kwenye Bhagavad-gītā imesemekana kuwa

avyakto 'kṣara ity uktas
tam āhuḥ paramāṁ gatim
yaṁ prāpya na nivartante
tad dhāma paramaṁ mama
(BG 8.21)

Avyakta inamaanisha isiyo dhiirika. Sehemu kubwa ya dunia hii haija dhirika kwetu. Fahamu zetu hazija kamilika na kwa hiyo hatuwezi kuona hesabu ya nyota zote, au sayari zote kwenye ulimwengu huu. Kama kawaida tunapata taarifa yote ya sayari kwenye maadiko ya Vedasi. Amini Usiamini, lakini sayari zote muhimu ambazo tunajuwa, zimeelezwa kwenye maandiko ya Vedasi, sana sana kwenye Śrīmad-Bhāgavatam. Lakini kwenye mbingu ya kiroho ambayo iko juu ya mbingu hii ya dunia paras tasmāt tu bhāvo 'nyo (BG 8.20), lakini avyakta hiyo yaani mbingu ya kiroho isiyo dhiirika ndiyo paramāṁ gatim, inamaana kuwa mtu anafaa kutamani baada ya kufikia ufalme huo mkuu. Na baada ya kufikia ufalme huo mkuu, yaṁ prāpya, anaye fikia ufalme huo mkuu, na nivartante, kamwe harudi katika ulimwengu huu. N a mahali hapo ambapo ni makaazi daima ya Bwana, hapoa mahali ambapo kamwe hatuta rudi, hapo ndipo tunafaa ku... Swali lina weza kuulizwa kuwa, mtu atafikia vipi ufalme huu wa bwana? Hayo pia yameelezwa kwenye Bhagavad-gītā. Inasemekana katiaka sura ya nane mstari wa tanao, sita, saba, nane, njia ya kumfikia Mwenyezi Mungu au makaazi yake kuu imepeanwa hapo pia. Imesemekana hivi:

anta-kāle ca mām eva
smaran muktvā kalevaram
yaḥ prayāti sa mad-bhāvaṁ
yāti nāsty atra saṁśayaḥ
(BG 8.5)

Anta-kāle, mwisho wa maisha yetu, wakati wa kifo. Anta-kāle ca mām eva. Atakaye mfikiria Kṛṣṇa, smaran, kama anaweza kukumbuka. Mtu anaye aga, wakati wa kifo, kama atakumbuka umbo la Kṛṣṇa na kwa ukumbusho wa njia hii, akiaga mwili wake, basi hakika anafikia ufalme wa kiroho, mad-bhāvam. Bhāvam inamanisha mazingira ya kiroho. Yaḥ prayāti sa mad-bhāvaṁ yāti. Mad-bhāvam inamaanisha kama vile Mwenyezi Mungu aliye na asili ya kiroho. Kama tulivyo eleza hapo awali kuwa Mwenyezi Mungu yu sac-cid-ānanda-vigraha (BS 5.1). Ana umbo lake walakini umbo lake ni daima, sat, na imejawa na maarifa, cit na kujawa na furaha kuu. Je mwili wetu wakati huu ni sac-cid-ānanda kweli? Hapana. Mwili huu ni asat. Badala ya kuwa sat, ni asat. Antavanta ime dehā (BG 2.18), Bhagavad-gītā inasema kuwa mwili huu ni antavat, utaangamia. Na... Sac-cid-ānanda. Badala ya kuwa sat ni kinyume. Na badala ya kuwa cit, kujawa na maarifa, imejawa na ujinga. Hatuna maarifa ya ufalme wa kiroho, wala hatuna maarifa kamili ya ulimwengu huu. Kwa hivyo mambo mengi hatujui, kwa hivyo mwili huu imejawa na ujinga. Badala ya kujawa na maarifa imejawa na ujinga. Mwili unaangamia, imejawa na ujinga na nirānanda. Badala ya kujawa na furaha, imejawa na taabu. Taabu hizi zote tunazopitia duniani yana sababishwa na mwili huu.