SW/Prabhupada 1075 - Tuna tayarisha maisha yetu ijayo kwa vitendo tunavyo tenda katika uhai huu



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Tuna tayarisha maisha yetu ijayo kwa vitendo tunavyo tenda katika uhai huu Bwana anasama kuwa-kāle ca mām eva smaran muktvā kalevaram (BG 8.5). Anaye aga mwili huu kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu, Bwana Krishna, mara moja anapata mwili wa kiroho amabayo ni sac-cid-ānanda-vigraha (BS 5.1). Njia ta kuaga mwili huu na kupata mwingine katika dunia hii pia imepangwa. Mtu anaaga wakati ambapo mwili atakao chukuwa kwenye maisha yake ijayo imeamuliwa. Lakini hayo yanaamuliwa na wakuu waliyo na mamlaka. Kama vile kulingana na kazi yetu tunapandishwa cheo au kushushwa. Vile vile, kulingana na vitendo vyetu tuna... Matendo ya uhai huu unatayarisha nafasi yetu kwenye maisha ijayo. Tunatayarisha maisha yetu ijayo kwa vitendo vyetu kwenye uhai huu. Kwa hivyo ikiwa tutanaweza kutayarisha maisha yetu wakati huu ili kukuzwa kwenye ufalme wa Mungu, basi bila shaka, baada ya kuaga mwili huu... Bwana anasema yaḥ prayāti, anaye enda, sa mad-bhāvaṁ yāti (BG 8.5), mad-bhāvam... Anapata mwili kiroho sawia na Bwana. Kuna aiana tofauti ya waumini, kama tulivyo eleza hapo awali. Wabrahmavādī, paramātmavādī na waja. Kwenye mbingu ya kiroho au kwenye brahma-jyotir kuna sayari za kiroho, sayari zisizoweza kuhesabika, kama tulivyo jadili. Na nambari ya sayari hizo ni nyingi sana, nyingi kuliko malimwengu ya dunia hii. Dunia hia ni ekāṁśena sthito jagat (BG 10.42). Hii ni robo ya udhiirisho wa viumbe vyote. Robo tatu ya uumbaji ni dunia ya kiroho na kwenye robo ya uumbaji huo kuna malimwengu milioni kama hii tunayo hisi wakati kuhuu. Na kwenye ulimwengu mmoja kuna mamilioni na mabilioni ya sayari. Kwa hivyo kuna mamilioni na mabilioni ya jua, nyota na miezi kwenye dunia hii yote ilhali dunia hii yote ni robo ya uumbaji wote. Robo tatu ni udhiirisho wa mbingu ya kiroho. mad-bhāvam hii, anayetamani kuchanganyika na Brahman kuu, wanachanganyika na brahma-jyotir ya Mwenyezi Mungu. Mad-bhāvam inamaanisha kuwa brahma-jyotir pamoja na sayari za kiroho kwenye brahma-jyotir. Na waja wanaotaka kufaidi kwenye mshirikiano wa Bwana, wanaingia kwenye sayari za Vaikuṇṭha. Kuna sayari nyingi za Vaikuṇṭha zisizoweza kuhesabika, na Bwana, Mwenyezi Śrī Kṛṣṇa, kupitia upanuzi wake kama Nārāyaṇa aliye na mikono minne na majina tofauti, Pradyumna, Aniruddha, na Mādhava, Govinda... Kuna majina mengi ya Nārāyaṇa, mwenye umbo la mikono minne. Moja wapo ya sayari hizo amabayo pia ni mad-bhāvam kwenye dunia hio ya kiroho. Kwa hivyo waumini amabao katika mwisho wa maisha yao, anafikiria kuhusu brahma-jyotir au atafakari kuhusu Paramātmā au amfikirie Mwenyezi Mungu, Śrī Kṛṣṇa, kwa njia yoyote, ataingia kwenye mbingu hiyo ya kiroho. Bali ni waja pekee, wale amabao wamejizoesha kushirikiana na Mwenyezi Mungu, wanataingia kwenye sayari za Vaikuṇṭha au sayari za Goloka Vṛndāvana. Bwana anasema yaḥ prayāti sa mad-bhāvaṁ yāti nāsty atra saṁśayaḥ (BG 8.5). Hamna wasi wasi. Mtu hapaswi kuto amini. Iyo ndiyo swali. Kwa hivyo tunasoma Bhagavad-gītā maisha yote, lakini Bwana anaponena kitu ambacho hakiambatani na mawazo yetu, tunaikataa. Hiyo sio njia ya kusoma Bhagavad-gītā. Kama vile Arjuna alisema ya kwamba sarvam etaṁ ṛtam manye, Nimeamini yote uliyo nena. Vile vile sikia. Bwana anasema kuwa wakati wa kuaga dunia, atakaye mfikiria, iwe ni kama Brahman au Paramātmā au Mwenyezi Mungu bila shaka anaingia kwenye mbingu ya kiroho na hakuna ubishi kuhusu jambo hilo. Mtu hapaswi kuto amini. Na njia na sheria hiyo pia imepeanwa kwenye Bhagavad-gītā, vile ambavyo mtu anaweza kufikia ufalme huo wa kiroho kwa kumfikiria Mwenyezi wakati wa kuaga dunia tu. Kwa sababu njia ya ujumla imetajwa:

yaṁ yaṁ vāpi smaran bhāvaṁ
tyajaty ante kalevaram
taṁ tam evaiti kaunteya
sadā tad-bhāva-bhāvitaḥ
(BG 8.6)