SW/Prabhupada 1064 - Bwana anaishi ndani ya msingi wa roho ya kila kiumbe



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Ufahamu mkuu, utaelezwa kwenye Bhagavad-gita katika sura ambayo inaeleza kuhusu tofauti ya jīva na īśvara kṣetra-jña hii inaeleza kuwa Bwana pia fahamu, na majīva au viumbe pia wana fahamu. Lakini tofauti ni kuwa fahamu ya viumbe imo ndani ya mwili wake pekee, lakini fahamu ya Bwana imo ndani ya miili yote. Īśvaraḥ sarva-bhūtānāṁ hṛd-deśe 'rjuna tiṣṭhati (BG 18.61).

Bwana anaishi ndani ya msingi wa roho ya kila kiumbe, kwa hivo anafahamu miendo na vitendo vya jīva wote. Tusisahau hiyo. Imeelezwa kuwa Paramātmā, au Mungu mkuu anaishi ndani ya roho ya kila mtu kama īśvara, kama mtawala na anapeana mwelekeo. Anapeana mwelekeo. Sarvasya cāhaṁ hṛdi sanniviṣṭhaḥ (BG 15.15). Amekaa ndani ya roho ya kila mtu na anapeana mwelekeo kama anavyo taka. Kiumbe huo anasahau la kufanya. Kwanza kabisa anang'a ng'ana kutenda kwa njia fulani, alafu ananaswa kutokana na matendo na matokeo ya matendo hayo ya karma yake mwenyewe lakini baada ya kuacha aina moja ya mwili, anaingia kwenye aina nyingine ya mwili... Kama vile tuna weza kuacha aina moja ya nguo tukachukua nyingine, vivyo hivyo, imelezwa kwenye Bhagavad-gītā, ya kuwa, vāsāṁsi jīrṇāni yathā vihāya (BG 2.22). kama vile mtu anaweza kubadilisha nguo tofauti tofauti, vile vile viumbe pia vinaweza kubadilisha miili tofauti tofauti kuondoka kwa roho, na pia kubeba matendo na matokeo ya matedo hayo ya zamani. Kwa hiyo, matendo haya yanaweza kubadilika wakati ambapo kiumbe kitakuwa katika hali njema au timamu, na aelewapo aiana ya vitendo ambavyo anapaswa kufanya, atakapo fanya hivyo basi, matendo yake na matokeo ya matendo hayo yanaweza kubadilika. Kwa hivyo karma haiishi milele. Vitu vyengine kando na vifungu hivyo vitano- īśvara, jīva, prakṛti, kāla, na karma— hizi nne ziaishia milele, ilahali karma, haiishi milele.

Fahamu kuu inayojulikana kama īśvara, na tofauti ya fahamu hii kuu au Bwana, na kiumbe wakati huu ni kuwa. Fahamu ya Bwana pamoja na ile ya viumbe inapita fikra za kila kitu yaani transidentali sio ati fahamu hii iantotokana na kuungana na dinia. hiyo ni wazo potovu. Nadharia ya kuwa fahamu inatokana wakati fulani ambapo kuna muungano wa vifaa fulani vya kidunia haikubaliki kwenye Bhagavad-gītā. Fahamu inaweza kufunikwa na akisio la hali ya kidunia, kzma vile, mwangaza inapoakisiwa kupitia kioo yenye rangi fulani, inaweza kuonekana kumiliki rangi hiyo. Vivyo hivyo, fahamu ya Bwana haithiriki na mambo ya kidunia. Mwenyezi Mungo, kama vile Krishna anasema Anaposhuka duniani, fahamu zake hazi athiriki na mambo ya dunia Kama fahamu zake zingekuwa zina athiriwa na mambo ya dunia, angefaa kuongea kuhusu mada hii takatifu kwenye Bhagavad-gītā. Mtu haweza kuongea kuhusu maswala ya mbinguni bila kuwa huru kutokana na uchafuzi wa fahamu za kidunia. Kwa hiyo Bwana hakuwa amechefuliwa na mambo ya dunia. Lakini fahamu zetu wakati huu umechafuliwa na mambo ya dunia. Kwa hivyo Bhagavad-gītā inafunza kuwa, ni lazima tu usafishe huu uchafuko wa fahamu zetu, na katika hiyo fahamu safi, matendo ambayo tutatenda itupa furaha. Hatuezi kuacha kutenda matendo yetu. Ni kuwa matendo hayo yasafishwe Alafu hayo matendo safi yanaitwa bhakti. Bhakti inamaanisha kuwa yanaonekana kama matendo ya kawaida, lakini hayaja chafuliwa. Ni matendo iliyo safishwa. Kwa hivyo mtu wa mjinga anaweza kuona kuwa huyu mja anafanya kazi kama mtu wa kawaida, mtu mwenye marifa duni hajui kuwa matendo ya mja au ya Bwana, hayaja chafuliwa na fahamu chafu za kidunia, walakini fahamu iliyo takatifu. Kwa hiyo tunafaa kujua kuwa fahamu zetu zimechefuliwa na mambo ya kidunia.