SW/Prabhupada 0014 - Devotees Are So Exalted

Revision as of 05:14, 12 July 2019 by Vanibot (talk | contribs) (Vanibot #0023: VideoLocalizer - changed YouTube player to show hard-coded subtitles version)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)


The Nectar of Devotion -- Calcutta, January 30, 1973

Kwa mfuasi, Krishna yuko kweneye mikono yake. Ajita, jito 'py asau. Ingawa Krishna hawezi kushindwa, anapenda kushindwa na wafuasi wake. Huu ndio msimamo. Kama vile kwa raha zake, anajiweka katika hali ambayo anashidwa na Mama Yaśodā, Kushindwa na Rādhārāṇī, kushindwa na rafiki zake. Krishna alishindwa, na lilbidi ambebe rafikiye mgongoni. Wazi wazi, saa zingine tunaona mfalme anamweka mcheshi kati ya wa washirika wake, na saa zingine mcheshi huyo anamtusi mfalme na mfalme anafurahia. Mcheshi saa zingine... Kama vile kuna mcheshi maarufu Gopāla Bon, kule Bengal. Siku moja, mfalme alimuuliza, "Gopāla, tofauti yako na punda ni nini?" Kwa hivyo mara iyo iyo akapima umbali wake na mfalme. Akasema, "Ni futi tatu pekee, bwana. Tofauti ni futi tatu pekee." Kila mtu akaanza kucheka. Na mfalme akafurahia matusi hayo. Kwa sababu saa zingine inahitajika.

Kwa hivyo Krishna pia... Kila mtu anampongeza kwa cheo chake. Kila mtu. Hiyo ndio cheo cha Krishna - Mwenyezi Mungu. Kule Vaikuṇṭha kuna sifa tu. Hakuna kingine. Lakini Vṛndāvana Kṛṣṇa yuko huru kukubali matusi kutoka kwa wafuasi wake. Watu hawajui maisha ya Vṛndāvana. Kwa hivyo waja wana adhimishwa sana. Rādhārāṇī anaamuru, "Usimruhusu Krishna kuja hapa." Krishna hawezi kuingia. Anawasifu wale magopi wengine. "Tafadhali niruhusu niingie." "La, la. Hairuhusiwi. Nenda zako." Kwa hivyo Krishna anapenda hayo.