SW/Prabhupada 0001 - Expand to Ten Million



Lecture on CC Adi-lila 1.13 -- Mayapur, April 6, 1975

Prabhupada: Caitanya Mahaprabhu anasema kwa ācārya wote Nityānanda Prabhu, Advaita Prabhu na Śrīvāsādi-gaura-bhakta-vṛnda wote wanafuata amri za Sri Caitanya Mahaprabhu. kwa hivyo jaribu kufuata njia ya ācārya. Na maisha itakuwa na fanaka. Na Kuwa ācārya sio ngumu. Kwanza kuwa mfanikazi mwaminify kwa mwalimu wako wa kiroho. ufuate kwa makini chochote anachosema. Jaribu kumfurahisha na kueneza ujumbe wa Kṛṣṇa. Ni hayo tu, sio ngumu hata kamwe. Jaribu kufuata amri za mwalimu wako wa kiroho na kueneza ujumbe wa Krsna. Hilo ndilo amri la Lord Caitanya.

āmāra ajñāya guru hañā tāra' ei deśa
yāre dekha tāre kaha 'kṛṣṇa'-upadeśa
(CC Madhya 7.128)

"Kwa kufuata amri yangu, wewe kuwa guru." Na kama tutafuata kwa makini hii njia ya ācārya na tujaribu kwa uwezo wetu wote kueneza ujumbe wa Kṛṣṇa. Yāre dekha tāre kaha 'kṛṣṇa'-upadeśa (CC Madhya 7.128). Kuna aina mbili za Kṛṣṇa Upadesa. Upadesa inamaanisha amri. Amri Krsna anayopatiana pia ni Kṛṣṇa Upadesa, na amri kumhusu Krsna pia ni Krsna Upadesa. Kṛṣṇasya upadeśa iti kṛṣṇa upadeśa. Samāsa, śāsti-tat-puruṣa-samāsa. Na Kṛṣṇa viṣayā upadeśa, hiyo pia ni Kṛṣṇa upadeśa. Bāhu-vrīhi-samāsa. Hiyo ndio njia ya kukagua lugha ya sanskrit. Kwa hivyo amri ya Kṛṣṇa ni Bhagavad-Gita. Anatupatia amri mwenyewe. Kwa hivyo anayeeneza Krsna Upadesa, rudia tu Krsna analosema, na unakuwa ācārya. Sio ngumu hata kidogo, kila kitu kimesemekana hapo. Tunafaa turudie tu kama kasuku. Sio kabisa kama kasuku, kasuku haelewi anachosema, hurudia tu. Unafaa kuelewa maana pia; ama utawezaje kueleza? Kwa hivyo tunataka kueneza ujumbe wa Kṛṣṇa. Jitayarishe tu kurudia amri za Krsna vizuri sana, bila kugeuzaq maana. Na hapo mbele, labda saa hii kuna wafuasi elfu kumi. Tutaongezeka hadi elfu mia moja. Hiyo inatakikana, tena elfu mia moja hadi millioni moja, na millioni moja hadi millioni kumi!

Devotees: Haribol! Jaya!

Prabhupada: Na hatutakosa ācārya, na watu wataelewa ujumbe wa Krsna kwa urahisi. Kwa hivyo, fanya hiyo mpango. Na usijiskie sana. Fuata amri ya ācārya na ujaribu nkuwa bila kosa, na uwe umekomaa. Na itakuwa rahisi kupigana na māyā. Ndio Ācāryas wanafanya vita na vitendo vya māyā.