SW/Prabhupada 0025 - If We Give Genuine Thing, it Will Act
Conversation with Yogi Amrit Desai of Kripalu Ashram (PA USA) -- January 2, 1977, Bombay
Yogi Amrit Desai: Nina mapenzi kubwa sana kwako, na nikasema lazima nije nikuone.
Prabhupāda: Asante.
Yogi Amrit Desai: Nilikuwa naambia waumini. Nilisema kwamba wewe ni.
Prabhupāda: Mko na Dkt. Mishra?
Yogi Amrit Desai: Hapana hatuko na yeye. Nilikuwa naambia waumini wote hapa. nilisema kuwa Sri Prabhupada ndiye mtu wa kwanza kuleta ibada hapa Magharibi inapohitajika sana. Kwa sababu huko wako kwa kichwa sana,kufikiria, kufikiria, kufikiria. Hii njia ya mapenzi ni ya kushangaza sana.
Prabhupāda: Ona tu. Iwapo utatoa kitu halisi
Yogi Amrit Desai: Halisi kabisa.
Prabhupāda: Itakuja kutambulikana.
Yogi Amrit Desai: Hiyo ndio maana inaongezeka vizuri sana, kwa sababu ni halisi kabisa.
Prabhupāda: Na ni jukumu la Wahindi kupeana kitu halisi kwa watu. Hii ni para-upakara. Kabla yangu, Hao wahubiri wengine wengine wote walienda kuwadanganya.
Yogi Amrit Desai: Hapana, Waliogopa kupeana ukweli halisi kwa sababu waliogopa kwamba hawatakubaliwa.
Prabhupāda: Hawakuwa wanajua ni nini ukweli. (kicheko) Sio kuogopa. Mbona? Iwapo mtu ako katika jukwaa la ukweli, mbona ataogopa?
Yogi Amrit Desai:Hakika.
Prabhupāda: Hawakujua nini ukweli , kwanzia Vivekananda.
Yogi Amrit Desai: Njia yote, Kweli. Ona, baada ya wewe kuja... Nilikuwapo mwaka 1960. Nilianza kufunza yoga. Lakini baada ya wewe kuja nikaishiwa na woga wa kufunza ibada ya mapenzi na kuimba nyimbo. Sasa hivi tuna ibada kubwa sana katika msikiti, ibada kubwa nyingi sana. Na nilitoa heshima kwako kwa sababu nilikuwa naogop kupeana ukweli kwa sababu nilifikiria, "Hawa ni Wakristo. Hawatapenda ibada sana vile. Laikini umetenda muujiza. Mungu, Krsna, ametenda muujiza kukupitia. Inashangaza sana, muujiza mkubwa zaidi katika dunia. Nahisi tu nguvu sana juu ya hivyo.
Prabhupāda: Ni wema wako kwamba unatoa tamko hili. Iwapo tutapeana kitu halisi, itafanya.
Yogi Amrit Desai: Ukweli. Hivi ndivyo nafanya pia. Kila mtu... Tuko na karibu watu 180 wanaokaa kabisa kwa msikiti, na waote wanazoea maisha ya useja. Kila mtu huamka saa 4:00, and huwa wanalala saa 9:00. Na hata huwa hawaguzani wao wenyewe kwa wenyewe. Huwa wanalala katika sehemu tofauti. Huwa wanakaa katika uhusiano tofauti. Kila kitu kina mashaarti. Hakuna madawa ya kulevya, hakuna pombe, hakuna kahawa, hakuna vitunguu. Safi.
Prabhupāda: Nzuri sana. Ndio. Tunafuata hii.
Yogi Amrit Desai: Ndio.
Prabhupāda: Uko na Mungu yeyote?
Yogi Amrit Desai: Ndio. Mola Krsna na Radha ndio Mungu wetu. Mwalimu wangu ni Swami Kripalu-anandi. Ako...Karibu na Baroda ako na nyumba. Alifanya ibada yake kwa miaka ishirini na saba, na miaka kumi na mbili alikaa kimya. Miaka ya mwiho michache anaongea mara moja au mara mbilikwa mwaka kwa sababu watu wengi wanamuomba.
Prabhupāda: Anakariri majina ya mungu?
Yogi Amrit Desai: Huwa anakariri. Katika kimya chake, kukariri kwake kwa majina ya Mungu kumekubaliwa. Kwa sababu anasema...Unaposema jina la Mungu, Hio haiweziitwa kuvunja kimya. Kwa hivyo yeye hukariri majina ya Mungu.
Prabhupāda: Kimya inamaana hatutaongea upuzi. tutakariri Hare Krsna. Hio ndio kimya. Ilhali badala ya kupoteza wakati, kuongea kuhusu kitu ya dunia, wacha tukariri Hare Krsna. Hio ni nzuri. Na kimya ni mbaya. Acha upuzi; ongea kitu ya maana
Yogi Amrit Desai: Kweli! Hio ni ukweli.
Prabhupāda: Param drstva nivartate (BG 2.59). Param drstva nivartate. Iwapo mtu ataacha upuzi, basi param, Mkuu... Param drstva nivartate. Wakata uko na vitu nzuri, basi unaacha mambo chafu. Hivyo kila kitu ya dunia, hio ni chafu. vitendo, maarifa, yoga , zote ni za dunia. Vitendo, maarifa, yoga. Hata zile zitambulikanazo kama yoga, zote ni za dunia.