YO/Prabhupada 0008 - Krishna sowipe "baba gbogbo agbaye nimi"



Janmastami Lord Sri Krsna's Appearance Day Lecture -- London, August 21, 1973

Kwa hivyo kule India, watu wote wakuu, watakatifu, na maācārya, wamekuza maarifa haya ya kiroho vizuri sana kwa ukamilifu, na hatuchukui nafasi hii kujinufaisha. Sio ati maandiko na miongozi hii ni ya Wahindi au mabrāhmaṇa. Hapana. Ni ya kila mtu. Kwa sababu Krishna anasema

sarva-yoniṣu kaunteya
sambhavanti mūrtayaḥ yaḥ
tāsāṁ mahad brahma yonir
ahaṁ bīja-pradaḥ pitā
(BG 14.4)

Krishna anasema kuwa "Mimi ni baba ya kila mtu." Kwa hivyo, ana wasi wasi kutupa amani, furaha. Kama vile baba anataka kuona mto wake akiwa shwari na kupata furaha, vile vile, Krishna pia anataka kuona kila mmoja wetu akiwa na furaha na akiwa shwari. Kwa hivyo anakuja saa zingine. (BG 4.7) Yadā yadā hi dharmasya glānir bhavati. Hii ndio sababu ya kuja kwa Krishna. Kwa hivyo watumishi wa Krishna, wafuasi wa Krishna, lazima wachukue misheni hii ya Krishna. Wanafaa kuchukua misheni hii ya Krishna. Hio ndio mtazamo wa Caitanya Mahāprabhu.

āmāra ajñāya guru hañā tāra ei deśa
yare dekha, tare kaha, 'kṛṣṇa'-upadeśa
(CC Madhya 7.128)

Kṛṣṇa-upadeśa. Jaribu tu kuhubiri kile Krishna alicho sema kwenye Bhagavad-gītā. Hiyo ndio jukumu la wahindi wote. Caitanya Mahāprabhu anasema.

bhārata-bhūmite manuṣya janma haila yāra
janma sārthaka kari para-upakāra.
(CC Adi 9.41)

Kwa hivyo jukumu la wahindi ni para-upakāra. Jukumu la wahindi sio kutumia wengine. Hiyo sio tabia ya Wahindi. Historia ya wahindi ni kwa ajili ya para-upakāra. Na hapo awali, watu wote duniani walikuwa wakija India kujifunza kuhusu maisha ya kiroho. Hata Yesu Kristo alienda huko. Na kutoka China na nchi zingine. Hiyo ni historia. Na tunasahau rasilmali yetu. Ukatili wetu ni wa kiwango upi. Muungano mkubwa kama huu, Krishna consciousness, inaedelea dunia nzima, lakini wahindi wetu ni wakatili, serekali yetu ni katili. Wahaikubali. Huu ni msiba wetu. Lakini kwenye misheni ya Caitanya Mahāprabhu. Anasema Mhindi yeyote, bhārata bhūmite manuṣya janma, akiwa ni binadamu, lazima akamilishe maisha yake kwa kuchukua manufaa ya vitabu ya Vedasi na asambaze maarifa haya duniani kote. Hiyo ni para-upakāra. Kwa hivyo India inaweza. Kwa kweli wana wathamini. Hawa wazungu, Waamrika, vijana, wana thamini ukuu... Napata barua nyingi kila siku, vile ambavyo wamenufaika na muungano huu. Kwa kweli hiyo ni kweli. Inapeana maisha kwa mtu aliye kufa. Kwa hivyo ntawaomba hasa wahindi, hasa Mheshimiwa, tafadhali ungana nasi kwenye harakati hizi, na ujaribu kufanisi maisha yako na wengine. Hiyo ndio misheni ya Krishna, kushuka kwa Krishna. Asante sana.