SW/Prabhupada 0022 - Krishna Is Not Hungry

Revision as of 05:14, 12 July 2019 by Vanibot (talk | contribs) (Vanibot #0023: VideoLocalizer - changed YouTube player to show hard-coded subtitles version)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)


Lecture on SB 1.8.18 -- Chicago, July 4, 1974

Kṛṣṇa anasema, "Muumini wangu, kwa upendo," yo me bhaktyā prayacchati. Kṛṣṇa hayuko njaa. Kṛṣṇa hajakuja kwako kuchukua sadaka yako kwa sababu ana njaa. hapana. Hana njaa. Yeye ako kamili kibinafsi, na katika ulimwengu wa kiroho anatumikiwa, lakṣmī-sahasra-śata-sambhrama-sevyamānam, Anatumikiwa na mamia na maelfu ya miungu wa utajiri. Lakini Kṛṣṇa ni mwema sana, kwa sababu ukiwa mpendwa wa Kṛṣṇa sana, ako hapa kukubali sadaka yako. Hata kama wewe ni maskini wa maskini, atakubali chochote unaweza tafuta. majani kidogo, maji kidogo, mauwa kidogo. Sehemu yoyote ya dunia, mtu yeyote anaweza pata na apatie Kṛṣṇa "Kṛṣṇa, sina chochote cha kukupatia, mimi ni maskini sana. Tafadhali kubali hii." Kṛṣṇa atakubali. Kṛṣṇa anasema, tad aham aśnāmi, "Mimi nakula." Hivyo ile kitu muhimu ni ibada,upendo, mapenzi halisi.

Hivyo hapa imesemwa alakṣyam. Kṛṣṇa hawezionekana, Mungu hawezionekana na macho, lakini yeye ni mwema sana kwamba amekuja mbele yako, anaonekana kwa macho yako ya kawaida. Kṛṣṇa hawezionekana katika dunia hii, kwa macho ya kawaida. kama vile sehemu mojawapo ya Kṛṣṇa. Sisi ni sehemu mojawapo ya Kṛṣṇa. Viumbe vyote wanaoishi, lakini huwa hatuoni kila kiumbe. huweziniona, na huwa sikuoni. "Hapana, nakuona," Unaona nini? unaona mwili wangu. Halafu wakati roho imetoka kwa mwili, mbona unalia "Babangu ameenda"? Mbona baba ameenda?Baba amelala hapa. Basi umeona nini? Umeona mwili wa babako aliyekufa, sio babako. Kwa hivyo kama huweziona chembe ya Kṛṣṇa, roho, utaonaje Kṛṣṇa? kwa hivyo maandiko inasema, ataḥ śrī-kṛṣṇa-nāmādi na bhaved grāhyam indriyaiḥ (CC Madhya 17.136). Haya macho ya kawaida hayaweziona Kṛṣṇa, ama kuskia jina la Kṛṣṇa ,nāmādi. Nāma inamaanisha jina. Nāma inamaanisha jina, umbo, ubora na michezo. Vitu hizi haziwezieleweka kwa macho ama hisia au viungo vya kawaida. Lakini iwapo yatatakaswa, sevonukhe hi jihvādau, ikiwa yatatakaswa kwa njia ya ibada, unawezaona Kṛṣṇa wakati wowote na mahali popote. Lakini kwa mtu wa kawaida, Kṛṣṇa: hawezionekana. Kṛṣṇa ako kila mahali,Mungu ako kila mahali, aṇḍāntara-stha-paramāṇu-cayāntara-stham. Hivyo alakṣyam sarva-bhūtānām. Ingawa Kṛṣṇa ako nje na ndani, zote, bado hatuwezi kumuona isipokuwa tunamacho ya kumuona Kṛṣṇa. Hivyo hili kongamano la ufahamu wa Kṛṣṇa ni la kufungua macho ya kumuona Kṛṣṇa. Na kama unaweza muona Kṛṣṇa, antah bahih, basi maisha yako imefaulu. Kwa hivyo maandiko inasema kwamba, antar bahir. antar bahir yadi haris tapasā tataḥ kiṁ nāntar bahir yadi haris tapasā tataḥ kim Kila mtu anajaribu kuwa mkamilifu, lakini ukamilifu inamaana, wakati mtu anawezaona Kṛṣṇa ndani na nje. Huo ndio ukamilifu.