SW/Prabhupada 0021 - Why So Many Divorces In This Country
Lecture on SB 6.1.26 -- Honolulu, May 26, 1976
kwa hivyo hii ndio njia jumla ya maisha. kila mtu katika vitendo hivi vya dunia, na kanuni msingi za vitendo vya kifamilia. maisha ya kifamilia, kulingana na mfumo wa maandiko ya Veda, mahali popote, ni wajibu maishani kudumisha bibi, watoto. kila mtu anahusika. wao wanafikiria hii ndio wajibu pekee. "Kumudu familia, hilo ndilo jukumu langu. Kwa starehe kama inavyowezekana. hilo ndilo jukumu langu. mtu hafikirii ya kwamba jukumula namna hii linafanywa na wanyama pia. Wao pia wana watoto, na wanakula. Tofauti ni nini? kwa hivyo neno lilotumika hapa ni mūḍha. Mūḍha inamaanisha punda. Yule anayeshiriki katika hayo majukumu, bhuñjānaḥ prapiban khādan. Prapiban. Prapiban inamaanisha kunywa, na bhuñjānaḥ anamaanisha kula. wakati wa kula,wakati wa kunywa, khādan, wakati wa kutafuna, carva casya raja preya (?). Kuna aina nne ya vyakula. wakati mwingine tanatafuna, wakati mwingine tunalamba, wakati mwingine tunameza na wakati mwingine tunakunywa. Hivyo kuna aina nne ya chakula. kwa hivyo tunaimba catuḥ vidhā śrī-bhagavat-prasādāt. Catuḥ vidhā inamaanisha aina nne. Hivyo huwa tunatoa sadaka kwa Miungu vyakuka nyingi sana miongoni mwa hizi aina nne. kitu fulani kinatafunwa, kitu fulani kinalambwa, kitu fulani kinamezwa. Kwa namna hiyo.
Hivyo bhuñjānaḥ prapiban khādan bālakaṁ sneha-yantritaḥ. Baba na mama hutunza watoto, vile kuwapatia chakula. Tumeona Mama Yaśodā vile analisha Kṛṣṇa. Kitu kimoja tu. hii ndio tofauti. Tunalisha mtoto wa kawaida, kama wanavyofanya paka na mbwa lakini Mama Yaśodā analisha Kṛṣṇa. Njia sawa tu. Kwa njia hakuna tofauti, lakini mmoja anashughulika na Kṛṣṇa na mwingine anashughulika na mambo ingine. hiyo ndio tofauti. Wakati inalenga Kṛṣṇa, basi ni ya kiroho, na wakati haina mwelekeo ,basi hiyo ni ya dunia. Hakuna tofauti kati ya vitu vya dunia....Hii ndio tofauti.. Kuna... kama vile tamaa na mapenzi, mapenzi halisi. kuna tofauti gani kati ya tamaa na mapenzi halisi? Hapa tunachanganya, mwanamme na mwanamke, kuchanganyisha na tamaa, Na Kṛṣṇa pia anachanganyika na wasichana. kijuu juu inaonekana kuwa kitu sawa. hata hivyo tofauti ni nini? Hivyo tofauti hii imeelezwa na mwandishi wa kitabu Caitanya-caritāmṛta, kwamba nini tofauti kati ya tamaa na mapenzi halisi? hiyo imeelezwa. Amesema, ātmendriya-prīti-vāñchā-tāre bali 'kāma' (CC Adi 4.165), "Wakati nataka kuridhisha hisia zangu, hiyo ni tamaa." Lakini kṛṣṇendriya-prīti-icchā dhare 'prema' nāma, "Na wakati tunataka kuridhisha hisia za Kṛṣṇa, basi hiyo ni mapenzi halisi, prema." hiyo ndio tofauti Hapa katika dunia hii hakuna mapenzi halisi. kwa sababu mwanamme na mwanamke, hawana wazo kwamba, "Nikichanganyika na mwanamme, yule mwanamme anayeridhisha tamaa yake na mimi." Hapana. "Nitaridhisha tamaa yangu." Hii ndio kanuni ya kimsingi. Mwanamme anafikiria kuwa "nikihusiana na mwanamke huyu nitaridhisha tamaa ya hisia zangu," na mwanamke anafikiria kwamba "Kwa kuhusiana na mwanamme huyu, nitaridhisha tamaa ya hisia zangu." Na hivyo hii ni maarufu sana katika nchi za Kimagharibi, na mara tu kuna ugumu katika kuridhisha tamaa, mara moja utengano. Hii ni ya kisaikolojia, kwa nini utengano mwingi katika nchi hii. Chanzo sababu yake ni kuwa " Mara tu siridhiki, basi sitaki." Hii imetajwa kwa Śrīmad-Bhāgavatam: dāṁ-patyaṁ ratim eva hi. Katika umri huu, bwana na bibi inamaanisha kuridhishwa na ngono, kibinafsi. Kwa hakuna swali kwamba "Tutaishi pamoja; tutaridhisha Kṛṣṇa kwa kufunzwa jinsi ya kuridhisha Kṛṣṇa." Hiyo ndio harakati ya Ufahamu wa Kṛṣṇa