SW/Prabhupada 0024 - Krishna is so Kind

Revision as of 05:15, 12 July 2019 by Vanibot (talk | contribs) (Vanibot #0023: VideoLocalizer - changed YouTube player to show hard-coded subtitles version)
(diff) ← Older revision | Latest revision (diff) | Newer revision → (diff)


Lecture on SB 3.25.26 -- Bombay, November 26, 1974

Wakati Arjuna alikuwa anamuona Kṛṣṇa uso kwa uso, Kṛṣṇa alikuwa anafunza Bhagavad-gītā - Kuona Kṛṣṇa namna hiyo na kusoma Bhagavad-gītā, ni kitu sawa. Hakuna tofauti. Mtu fulani, wanasema kwamba "Arjuna alikuwa na bahati tosha kumuona Kṛṣṇa uso kwa uso na kuchukua maelekezo." Hio si sahihi. Kṛṣṇa, anawezaonekana mara moja, iwapo umepata macho ya kuona. Kwa hivyo imesemekana, premāñjana-cchurita...mapenzi na ibada. kitu sawa. Premāñjana-cchurita-bhakti-vilocanena santaḥ sadaiva hṛdayeṣu vilokayanti [Bs. 5.38]. nitasisimua hadithi moja kwa uhusiano huu, kwamba brāhmaṇa mmoja katika South India, katika msikiti ya Raṅganātha, alikuwa anasoma Bhagavad-gītā. Na alikuwa hajui kusoma. Hakuwa anajua Kisanskriti wala helufi yoyote, alikuwa hajasoma. kwa hivyo watu, majirani, walikuwa wanajua kwamba "Huyu mtu hajui kusoma, na anasoma Bhagavad-gītā." Anafungua Bhagavad-gītā, "Uh, uh," hivyo ndivyo alikuwa. Hivyo mtu fulani alikuwa anafanya utani, "Brāhmaṇa, unasoma vipi Bhagavad-gītā?" Aliweza kuelewa kwamba "Huyu mtu ananifanyia utani kwa sababu sijui kusoma." Hivyo kwa njia hii, Caitanya Mahāprabhu pia ikafanyika kuwa alikuwa anapitia hapo siku hiyo katika msikiti wa Raṅganātha Na aliweza kuelewa kuwa "Hapa kuna muumini." Hivyo akamwendea na kumuuliza, "Mpenzi brāhmaṇa,unasoma nini? Hivyo aliweza kuelewa kuwa "Huyu mtu hanifanyii utani." Kwa hivyo akasema, "Bwana, nasoma Bhagavad-gītā. Najaribu kusoma Bhagavad-gītā lakini sijui kusoma. Mwalimu wangu wa kiroho alisema "Ni lazima usome sura kumi na nane kila siku." Hivyo sina elimu yoyote. siwezi soma. Bado mwalimu wangu wa kiroho alisema, hivyo najaribu kufanya kulingana na agizo lake. Na ninafungua kurasa, hivyo tu. Mimi sijui namna ya kusoma." Caitanya Mahāprabhu akasema "Wakati mwingine na mwingine nimeona ukilia." Halafu, "Ndio, nalia." Unaliaje kama hujui kusoma?" "Hapana, kwa sababu ninapochukua kitabu cha Bhagavad-gītā, naona picha moja, kwamba Kṛṣṇa ni mwema sana kuwa amekubali kuwa dereva wa gari ya Arjuna. Yeye ni muumini wake. Hivyo Śrī Kṛṣṇa ni mzuri sana kwamba anaweza kubali nafasi ya mtumishi kwa sababu Arjuna alikua anaamuru, 'Weka gari yangu hapa,' na Kṛṣṇa alikuwa anamtumkia. Kwa hivyo Kṛṣṇa ni mzuri sana. Hivyo ninapoona hii picha kwa akili yangu ,nalia." Hivyo mara hiyo Caitanya Mahāprabhu akamkumbatia, kuwa "Unasoma Bhagavad-gītā. Bila elimu yoyote, unasoma Bhagavad-gītā." Alimkumbatia.

Hivyo hii ni.... Vile alikuwa anaona picha? Kwa sababu alikuwa anapenda Kṛṣṇa, haijalishi, iwapo angesoma aya hizo au la. Lakini alikuwa amezama katika mapenzi ya Kṛṣṇa na alikuwa anaona, Kṛṣṇa alikuwa amekaa hapo, na alikuwa anaendesha gari ya Arjuna. Hii inahitajika.