SW/Prabhupada 0020 - To Understand Krishna is not So Easy Thing
Arrival Lecture -- Miami, February 25, 1975
Kumwelewa Krishna sio kitu rahisi.
- manuṣyāṇāṁ sahasreṣu
- kaścid yatati siddhaye
- yatatām api siddhānāṁ
- kaścid vetti māṁ tattvataḥ
- (BG 7.3)
Kati ya maelfu na ma milioni yawatu, mmoja anatamani kuhimarisha maisha yake. Hakuna anayetaka. Kwa kweli hawajui maana ya kufanikiwa maishani. ustaarabu wa kisasa, kila mmoja anafikiria, "Nikipata bibi mzuri na gari zuri na nyumba nzuri, hiyo ni mafanikio." Hiyo sio mafanikio. Hiyo haikawii. Mafanikio ya kweli ni kutoka kwenye mtego wa māyā, Kumaanisha hii maisha ambayo inahusu kuzaliwa, kufa, kuzeeka na magonjwa. Tunapitia maisha mengi tofauti, na hii maisha ya ki binaadam ni nafasi nzuri ya kutoka kwenye nyororo ya kubadilisha mwili moja baada ya nyingine, Roho ni daima na yenye furahaa kwa sababu ni kiungo cha Mungu, sac-cid-ānanda, daima, imejawa na furaha na yenye maarifa. Kwa bahati mbaya, duniani tunabadilisha miili, lakini hatufikii kii kiwango cha maisha ya kiroho amabapo hakuna kuzaliwa wala kufa. Hakuna sayansi. Siku ile daktari alikuja kuniona Na unamasomo gani ya kueweza kuelewa kuhusu roho, na cheo chake? Kwa hivyo dunia nzima kwa kweli iko kwenye giza. Wanahamu ya kuishi kwa miaka sitini au mia moja, lakini hawajui kuwa tungali daima, kujawa na furaha na maarifa, na kwa sababu ya huu mwili wa kidunia tumewekwa katika hali ya kuzaliwa, kufa, kuzeeka na kugonjeka. Na hali hii inaendelea mara kwa mara.
Kwa hivyo Bwana Śrī Caitanya Mahāprabhu alitokea kwa neema yake kuu kwa sababu ya walio anguka, Krishna pia huja. Lakini Krishna hana huria huo. Krishna weka sheria kuwa "Kwanza kabisa jisalimu. Kisha ntakuongoza." Lakini Caitanya Mahāprabhu anahuruma zaidi kumshinda Krishna, ingawa Krishna na Caitanya Mahāprabhu, ni kitu kimoja. Kwa hivyo kwa neema ya Caitanya Mahāprabhu tunamwelewa Krishna kwa urahisi. Na huyo Caitanya Mahāprabhu yuko hapa. Sio ngumu kumuabudu. Yajñaiḥ saṅkīrtanaiḥ prāyair yajanti hi su-medhasaḥ. Kṛṣṇa-varṇaṁ tviṣākṛṣṇaṁ sāṅgopāṅgāstra-pārṣadam, yajñaiḥ saṅkīrtanam (SB 11.5.32). Kariri tu Hare Krishna mantra, na chochote utakacho toa, kumpatia Caitanya Mahāprabhu. Ni mkarimu sana. Haoni makosa. Kuabudi Radha-Krishna ni ngumu sana. Lazima tumwabudu kwa hofu na heshima. Lakini Caitanya Mahāprabhu amekuja kwa mapenzi yake kuokoa walionguka. Huduma kidogo, atatosheka. Atatosheka. Lakini usipuuze. Kwa sababu ni mkarimu sana na mwenye huruma, haimaanishi tusahau cheo chake. Yeye ni Mwenyezi Mungu Mkuu. Kwa hivyo tumpe heshima kuu sana, na mpaka sasa... Lakini uzuri ni kuwa Caitanya Mahāprabhu haoni makosa. Na kumwabudu, kumtosheleza ni rahisi sana. Yajñaiḥ saṅkīrtanaiḥ prāyair yajanti hi su-medhasaḥ. We tu kariri Hare Krishna mahā-mantra na ucheze, na Caitanya Mahāprabhu atafurahi sana. Alianzisha dansi yake na ukariri wake na hii ndio njia rahisi ya kumjua Mungu. Mpaka sasa... Ikiwezekana, masaa ishirini na nne. Kama hiyo haiwezekani, angalau mara nne, mara sita, kariri Hare Krishna mbele ya Caitanya Mahāprabhu, na utapata mafanikio maishani. Hii ni hakika.