SW/Prabhupada 1059 - Kila mmoja ana uhusiano flani na Bwana



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Pindi atakapo kuwa mja wa Bwana moja kwa moja atagundua uhusiano wake na Bwana. mada hii ni ndefu lakini inaweza kuelezwa kwa ufupi kuna njia tano ambazo mja anaweza kuhusiana na Mungu mkuu. Moja inaweza kuwa kama mja katika hali tulivu, mwengine anaweza kuwa mja kwenye hali iliyo na uhai mwengine anaweza kuwa mja mwenye kumiliki hisia za kirafiki mwengine anaweza kuwa mja mwenye kumiliki hisia za uzazi mwengine anaweza kuwa mja mwenye kumiliki hisia za kimapenzi Kwa hiyo Arjuna alikuwa mja mwenye kumiliki hisia za kiafiki Bwana anaweza kuwa rafiki bila shaka dhana ya huu urafiki na ule urafiki ambayo tunamiliki katika dunia una tofauti mkubwa. Huu ni urafiki unaopita fikira za zote za kibinaadam sio ati kila mtu atakuwa na uhusiano huu na Bwana. Kila mtu anayo uhusiani wake na Bwana na huo uhusiano unaamshwa na ukamilifu wa huduma ya ibada Wakati huu katika maisha yetu hatuja msahau Mungu Mkuu peke yake, istoshe tumesahau uhusiano wetu wa milele na Bwana Kila kiumbe kati ya mamilioni na mabilioni ya viumbe, kila moja wao ana uhusiano fulani wa milele na Bwana. Iyo inajulikana kama svarūpa. Svarūpa. nakupitia njia ya huduma ya ibada mtu anaweza kufumbua svarūpa yake. na hiyo hatua inajulikana kama svarūpa-siddhi, yaani ukamilifu wa msimamo halisi wa binaadam. Kwa hiyo Arjuna alikuwa mja na pia likuwa na ushusiano wa kirafiki.

Mungu mkuu Bhagavad-gītā ilielezwa kwa Arjuna, na aliikubali vipi? Hiyo inapaswa kutiliwa maanani. Jinsi ambavyo Arjuna alikubali Bhagavad-gītā imetajwa katika sura ya kumi.

arjuna uvāca
paraṁ brahma paraṁ dhāma
pavitraṁ paramaṁ bhavān
puruṣaṁ śāśvataṁ divyam
ādi-devam ajaṁ vibhum
āhus tvām ṛṣayaḥ sarve
devarṣir nāradas tathā
asito devalo vyāsaḥ
svayaṁ caiva bravīṣi me
(BG 10.12-13)
sarvam etad ṛtaṁ manye
yan māṁ vadasi keśava
na hi te bhagavan vyaktiṁ
vidur devā na dānavāḥ.
(BG 10.14)

Baada ya kusikiliza Bhagavad-gītā kutoka kwa nafsi ya Mungu mkuu Arjuna anasema ya kwamba amemkubali Krishna kama paraṁ brahma, yaani Mungu mkuu Kila kiumbe kina ukuu wake kama Brahman, lakini kiumbe kikuu au nafsi ya Mungu mkuu ndio kuu zaidi kushinda viumbe vyote. paraṁ dhāma. Paraṁ dhāma inamaanisha Yeye ndio tegemeo la kila kitu. Na pavitram. Pavitram inamaanisha kuwa Yeye ni roho safi hawezi kuchafuliwa na fikra za kidunia. Na pia ameitwa kwa jina kama puruṣam. Kumaanisha mkuu ambaye faida zote zinamjia, śāśvatam, śāśvata, inamaana kuwa mwanzoni, Yeye ndio mtu wa kwanza divyam, kupita mafikira yote; devam, Nafsi ya Mungu mkuu, ajam, ambaye hazaliwi kamwe, vibhum, mkubwa zaidi. Mtu anaweza asiamini kuwa Kṛṣṇa alikuwa rafiki ya Arjuna, kwa hivyo anaweza kosa kusema haya mambo yote kwa rafiki yake. Kutoa ukosevu huu wa imani katika mafikira ya msomaji wa Bhagavad-gītā, Arjuna amefumbua pendekezo lake kupitia kwa wamiliki walio na mamlaka. Anasema kuwa Bwana Krishna amekubalika kama Mungu mkuu sio naye pekee, bali, amakubalika na wamiliki wa mamlaka kama Nārada, Asita, Devala, Vyāsa. Hawa watu ni wakuu zaidi katika usambazaji wa maarifa ya Vedasi. Wanakubalika na walimu wote watangulizi. Kwa hivyo Arjuna anasema ya kwamba, "Maneno yote ulioniambia mpaka sasa, nimeyakubali kuwa kamilfu kabisa."