SW/Prabhupada 1067 - Lazima tukubali Bhagavad-gita bila kutafsiri, bila kukata matamshi



660219-20 - Lecture BG Introduction - New York

Kuna vifaa ambavyo viumbe vinaweza kutumia kumtambua Mwenyezi Mungu. Na uto kamilifu wote inaaonekana kwa ajili ya utokamilifu wa maarifa. Kwa hivyo Bhagavad-gītā ndiyo maarifa kamili ya hekima ya Vedasi. maarifa yote ya Vedasi haiwezi kuangamia. Kuna mifano mengi ambayo tunatumia kuchukulia maarifa haya ya Vedasi kuwa ya kuto angamia. Kwa mfano, vile Wahindi wanachukulia maarifa haya ya Vedasi kuwa kamilifu, haifai hapa Kama vile kinyesi cha ng'ombe ni kinyesi cha mnyama. Kulingana na smṛti au hekima ya Vedasi, anayegusa kinyesi cha mnyama ni lazima aoge kujisafisha. Lakini kwenye maandiko ya Vedasi, kinyesi cha ng'ombe ni safi. yaani mahali popote pachafu pana safishwa na mguso wa kinyesi cha ng'ombe. Mtu akidai kuwa kivipi mahali pamoja kinyesi cha mnyama kina semekana kuwa chafu, na kwingine inasemekana kuwa kinyesi cha ng'ombe ambayo pia ni kinyesi cha mnyama ni safi, hayo ni mawazo ambayo yanapingana. Inaweza kuonekana kuwa yanapingana, lakini kwa sababu ni kanuni ya Vedasi, tunakubaliana nayo na hatufanyi makosa kwa kukubaliana nayo. Mwana sayansi Daktari. Lal Mohan Gosal, alifanya utafititi wa kinyesi cha ng'ombe na akagundua kuwa kinyesi cha ng'ombe ni kinamiliki mchnaganyiko wote wa antiseptiki. Vile vile kwa udadisi wake amefanya utafiti wa maji ya mto Ganga Mawazo yangu ni kwamba maarifa ya Vedasi ni kamilifu kwa sababu inapiata mashaka na makosa yote. Na Bhagavad-gītā ndiyo kiini cha maarifa yote ya Vedasi. Kwa hivyo maarifa ya Vedasi hayawezi kuangamia. Inashuka kupitia mpangilio wa nidhamu kamilifu.

Kwa hiyo maarifa ya Vedasi sio kitu cha kufanyiwa utafiti. Kazi yetu ya utafiti sio kamilifu kwasababu tuna tafuta vitu vyote kwa kutumia fahamu ambazo hazija kamilika. Kwa hiyvo matokeo ya kazi yetu ya utafiti pia haikamiliki. haiwezi kukamilika. Tunapaswa kukubali maarifa iliyo kamili. Maarifa haya yana shuka, kama ilivyo semekana kwenye Bhagavad-gītā, tumeanza tu, evaṁ paramparā-prāptam imaṁ rājarṣayo viduḥ (BG 4.2). tunapaswa kupata maarifa hayo kutoka kwa chanzo cha maarifa hayo, kuanzia kwa Bwana mwenyewe alafu kupitia kwa mwalimu wa kiroho atokaye katika mfululizo huo wa orodha. Kwa hivyo Bhagavad-gītā imeongewa na Bwana mwenyewe. Na Arjuna, mwanafunzi wake, ambaye alipokea mafundisho ya Bhagavad-gītā, aliyakubali kama yalivyo bila kuondoa chochote. Hatukubaliwi kukubali sehemu moja ya Bhagavad-gītā alafu tukatae nyingine. Hiyo pia haikubaliwai. Ni lazima tuikubali Bhagavad-gītā bila utafsiri au undofu wowote, na pia bila mshiriko wetu wa kijinga katika maswala hayo, kwa sababu inafaa kutwaliwa kama maarifa kamili zaidi ya Vedasi Maarifa ya Vedasi yanapokewa kutoka kwa duru za kiroho kwa sababu neno la kwanza lilinenwa na Bwana mwenyewe Manano yaliyo nenwa na Bwana yanaitwa apauruṣeya, yaani manaeno amabayo hayajanenwa na mtu yeyote wa dunia hii amabaye ameambukizwa na makosa ma nne Kiumbe chochote duniani kinamiliki makosa manne maishani moja....ni lazima afanye makaosa mbili...lazima wakati mwingine awe katika hali ya udanganyifu tatu... ni lazima atajaribu kudanganya wengine, na nne...fahamu zake hazijakamilika kupitia misingi hiyo nne ya makosa, mtu hawezi kutoa habari kamili kuhusu maarifa yaliyo enea kote. Vedasi haziko hivyo. Maarifa ya Vedasi yaliwekwa ndani ya moyo wa Brahmā, kiumbe wa kwanza. Alafu Brahmā akaigawa kwa wana na wanafunzi wake kama alivyo yapokea kutoka kwa Bwana.